Trump: Kumbe urais ni ‘Msalaba’


WASHINGTON, DC

Donald Trump
ANAKUMBUKA udereva, anajihisi kuwa ndani ya kifukofuko, na anashangaa jinsi kazi yake mpya ilivyo ngumu.

Rais Donald Trump juzi alikumbuka siku zake 100 za kwanza Ikulu huku akikumbuka maisha yake kabla ya kuingia madarakani.

“Nilipenda maisha yangu ya nyuma. Nilikuwa na mambo mengi sana yakiendelea,” Trump aliliambia Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) katika mahojiano maalumu. “Hii ni kazi kubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Nilidhani itakuwa rahisi kuliko.”

Akiwa tajiri kutoka New York, Trump aliingia madarakani kwa mara ya kwanza alipoingia Ikulu Januari 20 baada ya kumshinda Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Hillary Clinton.

Zaidi ya miezi mitano baada ya ushindi wake na siku mbili kabla ya siku 100 za urais wake, uchaguzi bado umo akilini mwa Trump.

Katikati ya mazuungumzo juu ya Rais wa China, Xi Jinping, Rais alitulia kidogo ili akabidhi nakala za kile alichosema ndizo takwimu za sasa kutokana na ramani ya uchaguzi wa mwaka jana.

“Hapa, mnaweza kuchukua hiyo, hiyo ndiyo ramani ya mwisho ya idadi,” Rais huyo wa Republican alisema akiwa mezani ofisini mwake, akikabidhi ramani za Marekani na maeneo ambayo alishinda yakiwa yamewekwa alama nyekundu. “Ni nzuri, sawa? Nyekundu bila shaka ni sisi.”

Alikuwa na nakala kwa kila mwandishi kati ya watatu hao wa Reuters ofisini mwake.

Trump, ambaye alisema alizoea kutokuwa na faragha katika “maisha yake ya uzee,” alielezea mshangao wake wa jinsi anavyobanwa sasa. Na aliweka wazi kwamba anaanza kuzoea ulinzi wa saa 24 pamoja na udhibiti mwingine unaoendana na hali hiyo.

“Hakika unakuwa umo kwenye kifukofuko chako mwenyewe, kwa sababu unakuwa na ulinzi mkali vile, kiasi kwamba huwezi kwenda kokote,” alisema.

Rais anapoondoka Ikulu, kwa kawaida anakuwa ndani ya gari maalumu la limousine au SUV. Alisema anakumbuka jinsi alivyokuwa akijiendesha mwenyewe. “Napenda kuendesha,” alisema. “Hivi sasa siwezi kuendesha tena.”

Vitu vingi juu ya Trump havijabadilika kutoka usimamizi wa kibiashara na uandaaji vipindi vya televisheni akiendesha mambo yake kutoka ghorofa ya 26 ya jengo la Trump Tower jijini New York huku akitumia muda mwingi kwenye simu.

Amekuwa akiwasiliana na marafiki zake wa nje na wabia wake wa kibiashara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine chanya. Wasaidizi wake waandamizi wanasema wao wameachana na hali hiyo.

Rais huyo amekuwa katika mgongano na mashirika mengi ya habari tangu kampeni zake za uchaguzi na kuamua kutohudhuria Chakula cha Usiku cha Waandishi wa Habari wa Ikulu jijini Washington, D.C., kwa sababu alihisi hakutendewa haki na vyombo vya habari. 

“Nitakuja mwakani, kwa hakika,” Trump alisema alipoombwa kama atahudhuria hafla hiyo siku zijazo.

Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Ikulu. Mwandishi wa Reuters, Jeff Mason ndiye rais wake.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo