Wananchi Gongolamboto walilia daraja


Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kunusuru daraja linalounganisha Gongolamboto na Machinjio ya Pugu kwani liko hatarini kusombwa na maji.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na wakazi wa Pugu Machinjioni wakisema hatua za haraka zisipochukuliwa mawasiliano ya wananchi wa Gongolamboto yatakatika na kuwa adha kwao.

"Tunaomba Manispaa ilifanyie ukarabati daraja hili ambalo kwa sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha," alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.

Mkazi mwingine Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo litasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi watakaolazimika kutumia njia ndefu kufika shuleni kwa kuwa wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.

Jithada za kumpata Diwani wa eneo hilo kuzungumzia suala hilo zilishindikana baada ya simu yake kutopatikana.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo