Kesi ya vigogo MSD kusikilizwa leo


Grace Gurisha

KESI ya matumizi mabaya ya madaraka inayowakabili vigogo wawili wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha ushahidi, baada ya washitakiwa kusomewa maelezo yao ya awali.

Kesi hiyo namba 102 ya 2017 itasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, ambapo upande wa Jamhuri utawakilishwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru.)

Vigogo hao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Cosmas Mwaifwani na Kaimu Meneja Ununuzi, Frederick Nicolaus, ambao waliposomewa maelezo hayo walikubali majina yao na vyeo vyao, lakini wakakana tuhuma zinazowakabili.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa  kuwa kati ya Machi mosi na 19, 2013 wakiwa makao makuu ya MSD Temeke, Dar es Salaam, kwa nafasi zao walitumia madaraka vibaya kuandaa, kusaini  mkataba namba moja wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/1011/60  wa Machi mosi, 2013.

Pia wanadaiwa kuwa waliandaa waraka wa mwito namba 2 wenye kumbukumbu MSD/003/Q/G/2010/2011/60 wa Machi 19, 2013 na kuisababishia kampuni ya H.H. Hillal & Company Limited kupata manufaa ya Sh 482,266,000.

Baada ya kusomewa mashitaka, walikana na kuwa nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo