Sheria Hifadhi ya Ngorongoro kurekebishwa


Joyce Kasiki, Dodoma

Hifadhi ya Ngorongoro
WIZARA ya Maliasili na Utalii iko kwenye maandalizi ya awali ya kufanya marekebisho ya sheria iliyoanzisha eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ramo Makani alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Molel (CCM).

Katika swali lake, Molel alitaka kujua ni lini Serikali  itarekebisha sheria hiyo ya mwaka 2002 ili wananchi wapate maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.

Makani alisema ni muhimu kuzingatia, kwamba katika marekebisho hayo, Serikali itaweka msisitizo zaidi katika kuboresha shughuli za uhifadhi wa eneo la Ngorongoro ili ibaki katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia.

Alikiri kuwa sheria hiyo iliyotungwa mwaka 1959 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 inazuia wananchi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kulima bali kufuga peke yake.

Hata hivyo, alisema kabla ya mchakato huo utatanguliwa na shughuli za kitaalamu  ambapo ndani ya wiki moja kikosi cha sensa kwa watu Ngorongoro kitafanya kazi ili marekebisho hayo yawe ya kisayansi.

"Wakati Mamlaka hiyo inaanza ilikuwa na watu 8,000 lakini
hadi mwaka 2011 kulikuwa na zaidi ya watu 89,000 , hivyo mabadiliko ya sheria hiyo yanatakiwa kuangalia vitu mbalimbali ikiwamo idadi ya watu," alisema Makani.

Makani alisema katika mwaka wa fedha ujao, mchakato wa sheria hiyo utaanza na kukamilika ndani ya kipindi hicho.

Alisema kutokana na zuio la kisheria la kulima, wakazi wa
Ngorongoro ambao kwa asili ni wafugaji, wamekuwa
wakitengewa bajeti ya kununulia mahindi ambapo takribani tani 3,600 hugawiwa bila malipo kila mwaka kwa matumizi ya chakula hususan kwa wenye kipato ca chini na wasiojiweza na kwa wenye uwezo huuziwa kwa bei nafuu.

"Ili kukabiliana na changamoto ya chakula, mwaka 2007 Mamlaka ilianza mchakato wa kupata maeneo ya kilimo
nje ya hifadhi kwa kutenga bajeti na kuwezesha mradi wa JEMA katika kata ya Oldonyosambu, ukiwa na lengo la kuondoa wahamiaji haramu walioingia ndani ya Hifadhi.  

Pia alisema malengo yalikuwa ni kutoa fursa kwa wenyeji halali ambao wangependa kufanya shughuli za kilimo na ufugaji nje ya Hifadhi.



Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo