Serikali kushirikiana na sekta binafsi kuhudumia


Mwandishi wa MAELEZO, Dodoma

Dk Hamis Kigwangalla
SERIKALI imeanza hatua za awali za uainishaji gharama, uandaaji mfumo mbadala na upembuzi wa kina wa aina ya ubia, ili kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji huduma za uchunguzi wa magonjwa.

Hayo yalisemwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, wakati akijibu hoja za wabunge, Dodoma.

“Kutokana na kukua kwa kasi kwa Sayansi na Teknolojia ya Uchunguzi wa Magonjwa, Wizara inakubaliana na wazo hili juu ya kuangalia namna nzuri ya kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji huduma hizi,” alisema Kigwangalla.

Alisema kwa kuanzia sasa, Wizara yake inafikiria kuanzisha ushirikiano kwa kupitia ukodishaji vifaa ambapo Serikali itakodisha mashine hizo ambazo zitakuwa za mbia na Serikali haitahusika na ununuzi, ufungaji na matengenezo kinga ya mashine hizo.

Alibainisha kuwa katika mfumo huo, Wizara yake itakuwa na jukumu la kusimamia utoaji huduma na itapata gawio lake kutokana na makusanyo yatokanayo na uchangiaji huduma kulingana na mkataba.

“Ni imani ya Wizara kuwa kutumia mfumo wa ubia na sekta binafsi (PPP) huduma za uchunguzi wa magonjwa zitaimarika na kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama,” alisema Kigwangalla.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo