Wabunge Kenya wamtembelea Lowassa


Mwandishi Wetu 

Edward Lowassa
WABUNGE 11 kutoka Kenya na wageni mbalimbali jana walimtembelea Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kijijini kwake Ngarash mkoani Arusha. 

Huku wakiongozana na vikundi vya wajasiriamali vya mkoani humo, wabunge hao walifanya mazungumzo na mbunge huyo wa zamani wa Monduli ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, alishika nafasi ya pili nyuma ya Rais John Magufuli. 

Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alithibitisha ugeni wa wabunge hao na kubainisha kuwa walikuwa na ujumbe maalumu kwa Lowassa. 

Wabunge hao wanamtemebela Lowassa katika kipindi ambacho Kenya inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu Agosti. 

Licha ya Liongo kutopatikana kufafanua lengo la ziara hiyo, duru za siasa zinaeleza kuwa wabunge hao walikwenda kuchota uzoefu wa uchaguzi kwa Waziri Mkuu huyo, ambaye katika uchaguzi wa mwaka juzi alitoa upinzani mkali kwa chama tawala CCM. 

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47 akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97. 

Matokeo hayo yalimfanya Rais Magufuli kupata asilimia chache ya kura kuliko wagombea wengine wa CCM, lakini licha ya uchache huo amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo