Ripoti ya uchumi Tanzania kuzinduliwa leo


Suleiman Msuya

Bella Bird
BENKI ya Dunia (WB), leo itazindua ripoti ya tisa ya hali ya uchumi nchini katika hafla itakayofanyika Dar es Salaam.

Taarifa ya benki hiyo kwa vyombo vya habari kupitia Ofisa Mawasiliano wake, Loy Nabeta jana, ilieleza kuwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB), Bella Bird, atazindua ripoti hiyo huku Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akiwa mgeni rasmi.

Nabeta alisema WB imekuwa na utaratibu wa kutoa ripoti ya uchumi kwa nchi wanachama, Tanzania ikiwa moja wapo.

Alisema wadau watashiriki kuijadili ikiwa ni pamoja na kupitia sera mbalimbali ambapo kwa pamoja watakuja na maoni ya hali ya uchumi nchini.

Ofisa Mawasiliano huyo alisema kila ripoti inayotolewa imekuwa ikijadili sekta husika kwa kina ambapo kwa hii itajikita zaidi kuonesha mchango wa sekta ya fedha nchini.

“Katika uzinduzi huo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa WB pia watakuwapo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Ushauri ya Rex, Dk Hawa Sinare, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Afrika, Ahmed Lussasi.

Wakati ripoti hiyo ya uchumi ikitarajiwa kuzinduliwa leo ripoti ya mwaka jana inaonesha uchumi wa Tanzania Mei mwaka jana ulikua kwa asilimia 6-7.

Ripoti ya mwaka jana ilionesha mfumuko wa bei ulikuwa unapungua kuanzia Januari kutoka na ununuzi mbalimbali.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo