Samia: Tanzania ni salama kwa uwekezaji


Mwandishi Wetu

Mama Samia
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi salama kwa uwekezaji Afrika.

Amesema hilo linasababishwa na kutokuwa na matatizo ya migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa mali za wawekezaji ikilinganishwa na nchi zingine Afrika.

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua maonesho ya kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Dar es Salaam.

Pia alikaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Ufaransa kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa kwenye kilimo, nishati, utalii na usafiri kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Makamu wa Rais alisema maonesho hayo ambayo yataambatana na kongamano la kibiashara la nchi hizo mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa kubadilishana uzoefu katika masuala ya kibiashara na uwekezaji.

Alieleza kuwa katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda Tanzania haiwezi kufanya kazi hiyo peke yake, bali kwa kushirikiana na mataifa makubwa yenye teknolojia ya kisasa katika uwekezaji ikiwamo Ufaransa.

Aliwahakikishia wawekezaji wote wanaokuja nchini kuwa Serikali itafanya kila linalowezekana kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji.

Alisema ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji Afrika, Serikali imeendelea kutenga bajeti ya kutosha kuimarisha miundombinu ya bandari, reli, barabara, usafiri wa anga ili kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini.

Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili kwa kina fursa za uwekezaji nchini hasa kwenye nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano na miradi ya maendeleo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo