Watatu wafa njaa Serengeti


Joyce Kasiki, Dodoma

Marwa Chacha
WATU watatu akiwamo mama na watoto wake wawili, wamefariki dunia katika Jimbo la Serengeti mkoani Mara baada ya kula mihogo iliyodhaniwa kuwa na sumu kufuatia ukosefu wa chakula ubalikabili jimbo hilo.

 Mbunge wa Serengeti Marwa Chacha (Chadema) alibainisha kutokea kwa vifo hivyo jana wakati akiomba mwongozo wa Spika, bungeni mjini Dodoma.

“Hali ni mbaya watu wanakufa Serengeti. Katika Mkoa wote wa Mara, debe moja la mahindi linauzwa kati ya Sh. 25,000 na Sh. 30,000” alisema Marwa.

Alisema hali hiyo ya uhaba wa chakula pia imesababishwa na tembo ambao wamekuwa wakila mazao ya wananchi kila yanapofikia wakati wa kuvunwa.

Alieleza kusikitishwa na kitendo cha Serikali kushindwa kutoa chakula cha bei nafuu kwa wananchi wakati katika baadhi ya maghala ya Serikali kuna chakula kimerundikana na kinaoza wakati wananchi wanakufa kwa njaa.

"Tumeenda Shinyanga kwenye ghala la Serikali, tumekuta  mahindi yanaoza, lini mahindi hayo yanatumika kama  siyo wakati huwa njaa," alihoji Marwa

Katika mwongozo wake aliliomba Bunge liache kujadili shughuli zilizopangwa kwa siku hiyo na kujadili hoja yake ya uhaba wa chakula.

"Naomba tuahirishe hoja, ili tujadili suala la njaa, sisi hatutaki chakula cha njaa, tunataka chakula cha bei nafuu,"alisema. 

Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson alivitaka vyombo vinavyohusika kufuatilia suala hilo na kulipatia ufumbuzi huku akitaka chakulaki.ichopo kwenye maghala kipelekwe kwa walengwa.

"Waziri wa kilimo yupo hapa na Bunge lilishahakikishiwa kwamba chakula kipo na hayo mahindi yanayooza  yapelekewe kwa wahitaji," alisema Dk.Tulia


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo