TRA yapiga kufuli ofisi TFF


Asha Kigundula

Ofisi za TFF
OFISI ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimefungwa na kampuni ya udalali kwa kushindwa ku­malizia kulipa deni ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mchezo kati ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Brazil mwaka 2010 na kodi ya mishahara ya makocha, Jan Poulsen na Kim Poulsen raia wa Den­mark.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8, mchana baada ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ilala na kampuni ya udalali ya Yono, kufika katika ofisi hizo na kuamuru wafanyakazi watoke na wao kua­mua kufunga ofisi hizo.

Ofisa mmoja wa TFF ambaye hakutaka jina lake lita­jwe, jana aliliambia Jambo Leo maofisa hao walipofika katika ofisi hizo waliwaambia watoke, nao wakatii kabla ya kufunga.

Alisema hatua hiyo imechukuliwa wakati Jumatatu wiki hii viongozi wa juu walipunguza deni kwa kulipa sh.milioni 250, kisha sh. milioni 40 siku iliyofuata.

TRA awali Machi 31 mwaka jana ilikamata magari ma­tano ya TFF pamoja na kufungia akaunti za TFF ambazo zilikuwa na fedha zaidi ya sh. milioni 400 ambazo zili­chukuliwa kwa ajili ya kufidia deni hilo.

Deni hilo la sh. milioni 1.6 lilitokana na kodi ya mechi kati ya Tanzania na Brazil iliyoandaliwa na serikali, iki­wa ni pamoja na kodi za mishahara ya makocha waki­geni ambao waliwahi kufundisha timu za Taifa, Taifa Stars.

Mwaka jana zilipofungwa akaunti hizo, kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) kilichokuwa katika safari yake kwa ajili ya mich­ezo ya kirafiki katika nchi za Burundi na Rwanda kilia­hirisha kutokana na kukosa posho za wachezaji na gharama za kambi.

Kwa sasa Serengeti Boys iko kambini kujiandaa kush­iriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) yatakayofanyika Gambia Mei mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo