Majina Bodi mpya CUF yawasilishwa Rita


Suleiman Msuya

Profesa Lipumba na Maalim Seif
BARAZA Kuu la CUF limewasilisha majina ya wajumbe wa Bodi yake mpya ya wadhamini kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma, Salim Biman alibainisha hayo jana katika taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari.

Alisema mapendekezo ya uteuzi wa wajumbe hao yalipokewa na Baraza Kuu la CUF kwenye kikao chake yakiwa ajenda namba 4(A) ili kukidhi matakwa ya Katiba Mpya ya CUF toleo la mwaka 2014 Ibara ya 98(1), (2), (3), (4), (5), na (6).

Diman alisema baada ya mjadala wa kina, Baraza Kuu lilipitisha majina ya wajumbe tisa wa Bodi ambao ni Abdallah Khatau, Ali Mbarak Suleiman, Mohamed Nassor Mohamed na Dk Juma Ameir Muchi.

Wengine ni Mwanawetu Said Zarafi, Blandina Mwasabwite,  Yohana Mbelwa, Mwana Masoud na Zumba Kipanduka.

Mkurugenzi huyo alisema hatua hiyo ni muhimu kwa chama iliyofanyika jana baada ya kukamilisha hatua zote za kikatiba za CUF, sheria za nchi na mikakati ya kuimarisha chama ili kukabiliana na wenye nia ovu dhidi ya CUF.

Alisema kikao hicho kilichofanyika Vuga, Mjini Unguja,  kilihudhuriwa na wajumbe halali 43 kati ya halali 53 na wajumbe watano kati yao hawakuhudhuria kwa udhuru kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kuwa nje ya nchi.

“Uteuzi huu wa Bodi mpya haubatilishi uamuzi wowote halali uliochukuliwa na Bodi ya awali na usajili huu umesimamiwa kikamilifu na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Nassor Mazrui na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi ambaye pia ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Joran  Bashange,” alisema.

Usajili huo unakuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kuunda Bodi ya Wadhamini mpya kwa madai iliyokuwapo muda wake umekwisha.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo