Gadiel Michael afurahia kuitwa Stars


Charity James

Gadiel Michael
BEKI wa kushoto wa Azam FC, Gadiel Michael, amesema amefurahishwa kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kwa mechi mbili za kimataifa.

Michael ni mmoja wa wachezaji walioitwa na Kocha wa timu hiyo, Salum Mayanga alipotangaza wachezaji 26 watakaoingia kambini Machi 19 kujiandaa michezo ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Alisema anamshukuru mwalimu kwa kuona umuhimu wake katika kikosi cha timu hiyo na kubainisha amefurahi na anaamini ni moja ya mafanikio yake katika soka.

“Ninafuraha sana, nimechezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 huko nyuma, najisikiavizuri kuitwa kwenye kikosi cha wakubwa, namshukuru kocha kwa kutambua uwezo wangu, naahidi kama ninavyofanya Azam FC nitaendelea kupambana kwa ajili ya kupigania namba kikosini,” alisema Gadiel.

Wachezaji wa Azam FC walioitwa kwenye timu hiyo ni saba, kipa Aishi Manula, mabeki Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Gadiel Michael, aliyeitwa kwa mara ya kwanza, viungo Himid Mao ‘Ninja’, pamoja na Frank Domayo ‘Chumvi’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambao wamerejeshwa kwenye kikosi hicho baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

Kwa idadi hiyo ya wachezaji, Azam FC ni miongoni mwa timu mbili zilizotoa wachezaji wengi sawa na Simba, huku kwa upande wa Yanga wakiitwa wanne pekee.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo