…Mwigulu aagiza aliyechomoa bastola asakwe


Mwandishi Wetu

Mwigulu Nchemba
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Ernest Mangu kumchukulia hatua mtu aliyemshikia bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nauye.

Juzi Nape aliitisha mkutano na vyombo vya habari lakini alionekana kuzuiwa na vyombo vya Dola ambapo baada ya kushuka alijitokeza mtu mwenye bastola ambaye alimwamuru arudi kwenye gari jambo ambalo lilimshangaza.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoiandika jana kupitia mtandao wake wa Instagram, Mwigulu alisema Nape si jambazi, ni Mtanzania, ni Mbunge, mjumbe wa NEC (Halmashauri Kuu ya Taifa) ya CCM, hana rekodi ya uhalifu.

Alisema kitendo cha mtu kumtolea bastola si cha kiaskari, si cha kitanzania na si cha ki-Mungu, na kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera anawaza mbali, ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.

“Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyenuia kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari,” alisema Nape. Alisema lazima atafutwe na kama ni askari sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.      

“Nasema lazima atafutwe, ajulikane ni nani achukuliwe hatua maana si jambo zuri kwa kitendo kilichofanyika cha kutoa silaha hata kama ni ukamataji alipaswa aseme sababu za kukamatwa.

“Nilishtushwa na mazingira ya tukio lile, nikajiuliza je ingekuwa eneo la kichochoroni ingetokea nini? Alisema Waziri huyo.

Juzi, kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari Nape alifika eneo husika na wakati akishuka kwenye gari alitokea mtu pembeni akamwamuru arudi ndani ya gari lakini baada ya kukaidi, alimtishia kwa bastola.

Hata hivyo, Nape hakutishika badala yake alishangaa na kucheka kwa kuwa ni kitendo ambacho hakukitazamia.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo