Bomoabomoa relini kuhamia Moro, Pwani


Emeresiana Athanas

OFISA Uhusiano wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), Catherine Mushi amesema ubomoaji wa nyumba zilizo kwenye hifadhi ya reli unatarajiwa kuhamia Morogoro na Pwani.

Aidha, amewataka Watanzania kushirikiana kulinda miundombinu ya reli na mali zote za Serikali.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, ofisa huyo alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa bomoabomoa iliyoanzia Dar es Salaam katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya Pugu na Ubungo.

Alisema katika mikoa hiyo, notisi ya siku 30 inatarajia kwisha Aprili 3   na hivyo ubomoaji unatarajia kuanza Aprili 10 katika mikoa mingine.

"Notisi katika mikoa hiyo imekwisha na tayari wamepewa taarifa. Katika hatua hii kumekuwa na malalamiko ya wananchi, lakini tunashukuru wanapisha licha ya kulalamika," alisema.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wote wanaoendelea kuishi kwenye   hifadhi za reli kupisha ujenzi wa reli mpya ya kisasa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo