Wanafunzi waonywa kutumia dawa za kulevya


Ibrahim Kunoga, Tanga

SERIKALI imewatata wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari nchini kuacha kutumia dawa za kulevya ikieleza baada ya kufanya utafiti imegundua asilimia kubwa ya wanafunzi wameathirika na matumizi ya dawa hizo hali inayowafanya kushindwa kutimiza malengo yao.

Akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, tawi la Tanga pamoja na wadau mbalimbali, Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa, Mwanne Ismail Nchemba alisema wana ugomvi mkubwa wa dawa za kulevya.

“Kwenye mkusanyiko wa watu hasa vyuoni na mashuleni, watumiaji wa dawa wamo,” alisema Mwanne wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika chuo hicho kilichopo Kange jijini Tanga.

Mwanne alisema malengo ya Taifa yatapotea iwapo wanafunzi hawatakuwa na msimamo wa maisha yao wenyewe akiongeza kwamba Serikali imeweka taratibu katika vyuo na sekondari kwa ajili ya kudhibiti dawa hizo viroba akieleza kwamba hata wanafunzi wa shule za msingi walikuwa wanatembea na viroba mfukoni.

"Tusidanganyane kwenye mkusanyiko wa wanafunzi kuna wanaovuta bangi na watumiaji wa dawa za kulevya. Pia suala la viroba tumeshaanza kulishughulikia, tuko hapa kwa malengo basi iwe vizuri tukazingatia malengo ya utumishi bora ili tuwe kioo katika jamii na serikali,” alisema Mwanne.

Kwa upande wake, mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Ukonga (Chadema) Waitara Mwita alisema taasisi nyingi za Serikali hazitumii nafasi ya vyuo vya utumishi ikiwemo kutokufanyika kwa semina elekezi hivyo kuna haja ya kubana matumizi kwani dunia inabadilika lazima watu waende na wakati.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo