…Wahariri wasisitiza msimamo wa kutomwandika


Mwandishi Wetu
Theophil Makunga

BODI ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imesisitiza vyombo vya habari kuendelea na msimamo wa kutoandika habari zozote ambazo kumhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Theophil Makunga baada ya kikao kilichofanyika Dar es Salaam ambapo wajumbe walisisitiza msimamo huo hadi Makonda atakapotambua kosa lake na kuomba radhi.

Alisema TEF ilijadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu ilipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu huyo ambapo hadi jana waliona kuwapo mshikamano.

“Bodi ilipitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia kuwa zinaridhisha hivyo tunawaasa wahariri na wanahabari kuendelea hivyo hivyo,” alisema.

Bodi iliwapongeza wahariri waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki hiyo nzima.

Aidha, alisema Bodi iliwataka viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga mkono msimamo huo ili kuwa fundisho kwa kiongozi huyo.

Makunga alisema Makonda amewekewa vikwazo maalumu kwa mikutano atakayoandaa au matukio atakayoongoza habari zake hazichapishwi.

Alisema Bodi ilikipongeza kituo cha Clouds Media kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo huo.

Aidha, alisema Bodi pia iliwasiliana na uongozi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.

TEF na UTPC kwa pamoja walitoa tamko la kutoandika habari yoyote ya Makonda baada ya kuvamia Clouds Media akiwa na askari wenye silaha usiku jambo ambalo halikubaliki katika nchi zinazosimamia misingi ya sheria na utawala bora.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo