Kizimbani kwa kumpa mimba mwanafunzi


Jemah Makamba

MKAZI wa Ukonga, Dar es Salaam, Rashid Ramadhan, amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala akituhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 15.

Akisowa mashitaka hayo juzi, mbele ya Hakimu Adelf Sachore, mwendesha mashitaka, Munde Kalombola alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 16 mwaka jana Ukonga, Mombasa ambapo pia alimkatisha masomo yake.

Baada ya kusomewa mashitaka mshtakiwa alikana kutenda kosa ambapo mwendesha mashitaka alisema upepelezi wa kesi hiyo haujakamilika lakini mshtakiwa ana haki ya dhamana kama atakidhi masharti atakayopewa.

Hakimu alisema dhamana ya mshitakiwa ni wadhamini wawili wenye ajira kwenye taasisi inayotambulika, ambapo watasaini ahadi ya Sh milioni mbili kila mmoja.

Mshitakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Aprili 6 kesi hiyo itakapotajwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo