Makamba: Ziwa Jipe kutangazwa eneo nyeti


Lulu Mussa, Kilimanjaro

ZIWA Jipe liko hatarini kutoweka ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kulinusuru.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba alibainisha hayo alipofanya ziara ya kukagua ziwa hilo ambalo sehemu kubwa imezungukwa na magugu maji.

Waziri Makamba amesema ni lazima kuwepo mpango wa muda mfupi na muda mrefu kulinusuru na kwamba kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) ameazimia kutangaza kuwa eneo hilo ni nyeti kimazingira.

"Tutatanga eneo hili kuwa eneo nyeti kimazingira na tutaweka masharti ya matumizi yake," alisema Makamba.

Waziri Makamba amesisitiza kuwa ni vema kunusuru ziwa hilo sasa maana ndani ya miongo 2-3 huenda ziwa hilo likatoweka

Alifafanua kwamba kutangaza kuwa eneo hilo kuwa nyeti kimazingira itasaidi katika kuandika maandiko mbalimbali ya miradi na kupata fedha kutoka kwa wadau na washirika wa maendeleo ili kulinusuru.

Makamba alisema ziwa hilo pia litawekwa chini ya uangalizi maalumu na kuweka masharti ya matumizi bora ya eneo hilo.

"Bila hifadhi ya mazingira hakuna maisha, na ukiyaharibu mazingira hakuna msamaha yatakuadhibu tu," alisema na kuongeza:

“Shughuli zozote za maendeleo iwe uvuvi, kilimo, utalii, mifugo kwa namna moja ama nyingine zinategema hifadhi endelevu ya mazingira.”

Katika hatua za muda mrefu Waziri Makamba amewataka wasimamizi wa Bonde la Pangani, Wizaya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kukutana mara moja kuandaa mpango na mtazamo wa pamoja wa kunusuru Ziwa Jipe.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo