Kizimbani kwa wizi wa kutumia silaha


Jemah Makamba

MKAZI wa Vingunguti, Dar es Salaam, Fadhili Omary (25) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akituhumiwa kuiba kwa kutumia silaha dhidi ya Asha Juma.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Eric Shija mbele ya Hakimu John Msafiri alidai kuwa mshitakiwa aliiba simu na fedha taslimu vyote pamoja vikiwa na thamani ya Sh 150,000.

Shija alidai mshitakiwa huyo alimkata mlalamikaji mkononi kwa panga baada ya kumpora simu hiyo Vingunguti kwa Mnyamani.

Baada ya kusomewa mashitaka mshitakiwa alikana huku mwendesha mashtaka akidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo kuomba siku nyingine ya kuendelea na kesi hiyo.

Kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana, mshitakiwa alirudishwa rumande hadi Aprili 6 kesi hiyo itakapotajwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo