Treni ya TRL kusafirisha mizigo Afrika Mashariki


Salha Mohamed

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRL) limezindua treni mpya ya mizigo itakayofanya safari zake Afrika Mashariki.

Uzinduzi huo ulifanyika Dar es Salaam jana ambapo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Shaban Kiko alisema treni hiyo yenye mabehewa 20 ilianza safari kwa kupeleka mizigo Burundi.

Kiko alisema TRL awali haikuwa na treni kubwa kama hiyo, hivyo wananchi watarajie kusafirisha mizigo kwa wakati na bei nafuu.

Aliongeza kuwa huduma hiyo imezinduliwa kwa wafanyabiashara na kampuni binafsi zenye shehena kubwa za mizigo zinazotosheleza mabehewa yote 20 ili kurahisisha kusafirisha mizigo moja kwa moja.

"Treni hii inayoanza safari zake leo (jana) imechukua mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam, iliyotoka China na kuipeleka Burundi," alisema Kiko.

Alifafanua kuwa treni hiyo itabeba malighafi ya chuma, mzigo unaosafirishwa na kampuni ya UBUCOM ya Burundi.

Alisema walitoa dola 3,056 za Marekani kwa behewa moja la mizigo ya kawaida na dola 3,024 kwa mizigo iliyofungwa kwenye kontena.

Aidha, safari hiyo itachukua siku mbili kuwasili Kigoma na siku moja Bujumbura huku shirika hilo likitajwa kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ya kawaida na inayohifadhiwa kwenye kontena.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo