Upelelezi kesi ya Wema mbioni kukamilika


Grace Gurisha

Wema Sepetu
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kukutwa na msokoto wa bangi inayomkabili msanii maarufu nchini, Wema Sepetu umeiambia Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umefikia hatua ya mwisho kukamilika.

Hayo yalielezwa jana na Wakili wa Serikali, Costantine Makula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Baada ya Makula kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi April 11 itakapotajwa tena. Pia Wema anatuhumiwa kukutwa na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Mbali na Wema, washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abbas (16), ambao wote wanashitakiwa kwa kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya.

Ilidaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4, nyumbani kwao Kunduchi Ununio, Kinondoni, Dar es Salaam.

Awali washitakiwa hao walikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Katuga alidai upelelezi wa haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Msanii huyo na wenzake wako nje kwa dhamana.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo