BancABC yazindua akaunti rafiki kwa wateja


Celina Mathew

BANCABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imezindua akanti maalumu ili kuhakikisha wateja wake wanapata riba hadi asilimia 16 kutokana na akiba yao huku ikieleza kuwa inathamini na kutambua mchango wao.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wafanyabiashara wa Kati, Joyce Malai aliyefafanua kuwa kwa hali ya kawaida amana za muda maalumu zimekuwa kivutio kwa wateja wa benki nyingi.

“Kwa kuanzia, amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida kwani unapata riba nzuri zaidi.          

“Faida nyingine ni uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia, kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe,” alisema.

Aliomba wasio na akiba kwenye benki hiyo kutumia nafasi hiyo kufungua akaunti ili kunufaika na faida zinazotolewa kwa wateja wake.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo