‘Babu’ kizimbani kwa kulawiti ‘mjukuu’


Jemah Makamba

MKAZI wa Vingunguti, Dar es Salaam, Amrani Hussain (59), amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala akituhumiwa kumlawiti kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Vingunguti.

Akisoma mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi Ritha Tarimo, mwendesha mashitaka Hilda Kato alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe tofauti Desemba mwaka jana Vingunguti.

Kato alidai kuwa mshitakiwa alimfanyia vitendo hivyo kijana huyo huku akijua ni kosa na ni kinyume cha sheria za nchi.

Baada ya kusomewa mashitaka mshitakiwa alikana na Hakimu kumpa masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini ahadi ya Sh milioni moja.

Hata hivyo, mshitakiwa alidai kuwa wadhamini wake hawakuwa wamefika mahakamani hapo hivyo Hakimu akaahirisha kesi hadi Aprili 4 itakapotajwa na mshitakiwa alirudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo