Msajili azuiwa kutoa ruzuku CUF

Mwandishi Wetu

Jaji Mutungi
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amezuiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa fedha za ruzuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake.

Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Wilfred Dyansobela baada ya jopo la mawakili wanaowakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF, kuwasilisha maombi ya kutaka kuzuiwa kwa fedha hizo kwani zilizotolewa awali, Sh milioni 369, haijulikani zilivyotumika.

Mawakili waliowasilisha ombi hilo ni Juma Nassor, Daimu Halfani na Hashim Mziray wakiiomba Mahakama kuzuia kutolewa fedha zingine hadi shauri namba 21/2017 dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ya kutoa fedha hizo kwa njia za wizi hadi litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Mawakili hao walisema fedha hizo hazikuwa kwenye mikono salama wala hakukuwa na udhibiti wowote CUF ikizingatiwa kuwa Profesa Lipumba alishavuliwa uanachama.

Wakili Nassor aliyewasilisha maombi hayo, alisisitiza kuwa kwa mazingira yaliyopo ni vema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa CUF sasa ziendelee kubaki serikalini.

Pia mawakili hao katika shauri hilo, waliiomba Mahakama amri hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji uamuzi wa Msajili kumtambua Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti, ambayo kwa sasa kesi hiyo imekatiwa rufaa/maombi ya kufanyiwa marejeo.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo