Aonya dhidi ya ulaji ovyo


Dalila Sharif

ULAJI ovyo wa vyakula visivyofaa husababisha ongezeko la uzito wa mwili (unene) na vitambi hali ambayo huweza kusababisha magonjwa kisukari, moyo, shinikizo la damu na hata saratani.  

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Ofisa Lishe wa Taasisi ya Lishe na Chakula Tanzania, Julieth Shine, akisisitiza kuwa ulaji wa vyakula usiofaa husababisha watu kuota vitambi hasa vyakula vyenye mafuta.  

Alisema ulaji wa vyakula usiotarajiwa husababisha unene uliopitiliza na kusababisha watu kuzidiwa na uzito wa miili uliopitiliza.  

“Hali hii inatokana na kukosa mtindo bora wa maisha, matumizi ya teknolojia ambayo yamefanya watu kutumia mashine kufanya kazi za nyumbani badala ya miili hivyo kukosa mazoezi,” alisema Shine.

“Ni vema kuzingatia mazoezi na kula kwa wakati kwa usiku mtu kula saa mbili na hivyo kusaidia kupunguza unene,” alisema Shine.

Alisema taasisi ina mipango ya kutoa elimu juu ya lishe   na kuendeleza mkakati wa Taifa wa kuzuia lishe isiyofaa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo