Mkwassa: Waarabu kufa Dar lazima


Charity James

KLABU ya Yanga, imesema hawatishiki na historia nzuri ya wapinzani wao katika mashindano ya kimataifa kikubwa wanachokiangalia ni kuhakikisha wanaanza vizuri nyumbani ili kupunguza mzigo ugenini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema timu yake imejipanga vyema kuelekea mchezo wao dhidi ya MC Alger kutoka Algeria na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa na hofu kutokana na ubora na uzoefu walionao wapinzani wao.

Alisema mpira ni kama mchezo wa kubahatisha, hivyo historia haiwezi kuwabeba wapinzani kama wengi wanavyochukulia na kubainisha dakika 180 ndizo zitakazoamua nani bora zaidi ya mwingine.  Mkwasa alisema licha ya wapinzani wao kuwa na historia nzuri, hawezi kuogopa hilo na amedhamiria kuifunga nyumbani ili watakapoenda kwao wasiwe na kibarua kigumu.

“Mechi kama hizi unapopata ushindi mzuri wa nyumbani, basi unapunguza mlima wa kuupanda ugenini. MC Alger ni timu nzuri na amekuwa bingwa wa Afrika, hivyo kila mtu atataka kuiona na tunawaheshimu kwa historia yao lakini tunakwenda kupambana kutafuta ushindi,” alisema.

Aidha Mkwasa alisema hadi sasa hajafahamu mechi hiyo itachezewa wapi ila muda utakapofika watuwataambiwa ni wapi ila wao popote watakapopangiwa wapo tayari kucheza.

“Muda ukifika tutawajuza wapi mechi itafanyikia kama ni hapa jijini au popote Tanzania. Kwa sasa bado hatujaamua lolote katika hilo, hivyo Uwanja wa Taifa unabaki kutambulika kama uwanja wa nyumbani,’’ alisisitiza Katibu huyo.

Kwa upande mwingine, aliwataka mashabiki na wadau wote wa soka nchini kuipa sapoti timu hiyo muda wote wa dakika 90 za mchezo bila ya kuogopa mbwembwe za wapinzano wao wanapokuwa wameuteka mpira miguuni mwao.

Yanga imeangukia mikononi mwa Waalgeria hao baada ya kufungwa na Zanaco katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo wapinzai wao walinufaika kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo