‘Trafiki pandeni miti ya matunda’


Mwandishi Wetu

Dk.Rehema Nchimbi
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi, ameagiza Askari Kikosi cha Usalama Barabarani kupanda miti ya matunda ili waweze kutumia matunda kwa ajili ya kuimarisha uono wao kwa ajili ya kutekeleza vizuri majukumu yao wakati wote wanapokuwa barabarani.

Dk. Nchimbi ametoa agizo hilo  hivi karibuni  wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyofanyika kwenye Kijiji cha Iguguno Wilaya ya Mkalama.

Alisema kiungo muhimu kwa askari wa usalama barabarani ni macho yenye uwezo wa kuona vizuri na kwa umbali wowote.

"Yapo matukio yametokea askari wa usalama barabarani anajitokeza barabarani anasimamisha gari la kiongozi,akitambua kuwa amesimamisha kiongozi,anaomba msamaha. Anajitetea kuwa hakujua kuwa gari husika limebeba kiongozi. Unamuuliza hata kama hukufahamu gari lina kiongozi, je hata bendera hujaiona?",alisema.

Dk. Nchimbi alisema kuwa askari wa aina hiyo ni wale ambao afya ya macho yao, imeathirika na kitendo cha kutokula matunda ya kutosha.

Akisisitiza, alisema ataanzia kukagua upandaji wa miti ya matunda kwa askari wa usalama barabarani,kisha baadae kwa askari wote,wakuu wa wilaya,viongozi wote wa serikali na wananchi kwa ujumla.

"Nitumie fursa hii kuwahimiza viongozi wa madhehebu ya dini,kuwahimiza kila kaya ya muumini  kushiriki kikamilifu 'operation' panda miti miwili ya miembe.Pia wakemee kiburi cha baadhi ya watu wanaoharibu mazingira kwa makusudi," alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo