‘Serikali iyafunge maduka yanayotengeneza nyavu bandia’


Joyce Kasiki, Dodoma

Abdallah Bulembo
MBUNGE wa kuteuliwa Abdallah Bulembo (CCM) ameitaka Serikali kuyafungia maduka yote yanayouza nyavu bandia, badala ya kuwachukulia hatua wavuvi wanaotumia nyavu hizo katika shughuli za uvuvi.

Bulembo alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza. Alisema wavuvi wanaotumia nyavu hizo za matundu madogo wamekuwa wakichukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kuchomewa nyavu zao huku maduka yanayouza nyavu hizo yakiendelea kutoa huduma.

"Je, ni lini Serikali itayafunga maduka hayo yanayouza nyavu feki na kuwasababishia wavuvi hasara?" alihoji Bulembo

Akijibu swali hilo,Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba alisema katika kupambana na uvuvi haramu imekuwa ikiwachukulia hatua watu wote wanaohusika katika kusababisha uvuvi haramu wakiwemo wauzaji, watunzaji na wazalishaji wa nyavu hizo, huku akieleza kuwa wakati mwingine wamekuwa wakifunga viwanda vinavyobainika kuzalisha nyavu hizo.

Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa viti maalumu Maria Kangoye (CCM) alitaka kujua ni lini Serikali itaimarisha huduma za ugani kwa kutoa mafunzo kwa kuongeza udahili wa maafisa ugani kutoka 1,200 hadi 2,500 kwa lengo la kuwa na maafisa ugani wengi na kuimarisha huduma za uvuvi na ufugaji samaki.

Pia alitaka kujua kama kuna mkakati wowote wa Serikali wa kuzishirikisha halmashauri nyingi katika mkakati wa kuhamasisha uchimbaji wa mabwawa na ufugaji wa samaki hasa katika maeneo yenye ukame ili kuongeza lishe bora na ajira kwa vijana.

Akijibu swali hilo, DkTizeba alisema,mkakati wa kuongeza udahili ili kuongeza Maafisa ugani wa uvuvi,ulianza kwa wizara kuimarisha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Feta) Katima Kampasi zake za Mbegani,Nyegezi,Kibirizi,na Mwanza.

Vile vile alisema ili kuongeza udahili na wanafunzi,Setikali itakamilisha ujenzi wa Kampasi za Mkindani (Mtwara) na Gabimori (Rorya) ifikapo mwaka 2019 ambapo kwa ujumla vyuo vyote vitadahili wanafunzi 2,000 kwa mwaka ikilinganishwa na 1,200 wanaodahiliwa hivi sasa kwa mwaka.

Dk.Tizeba alisema,vyuo hivyo vinzalisha wataalam wa uvuvi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada ambao hupata ajira Serikalini ,sekta binafsi na wengine hujiajiri wenyewe.

Kuhusu mkakati wa kuzishirikisha Halmashauri katika uchimbaji wa mabwawa alisema,wizara kwakushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa imechimba visima virefu 101 kwa ajili ya kujaza maji kwenye mabwawa ya kufugia samaki na malambo 1,381 kwa ajili ya kunyweshea mifugo ambayo pia hupandikizwa samaki.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo