Nusu ya Watanzania wanatumia tiba mbadala


Joyce Kasiki, Dodoma

Ummy Mwalimu
SERIKALI imesema asilimia 60 ya Watanzania wanategemea tiba inayotolewa na waganga wa tiba asilia.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la nyongeza la  Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph  Kasheku  (CCM)   aliyeihoji Serikali kwa nini haitambui mchango wa waganga hao na ikawapa elimu ya masuala ya afya.

"Hivi siku zote watu wamekuwa wakiwasemea wasanii kwamba wanatumika wakati wa uchaguzi na baada ya hapo wanasahaulika,lakini kwa kipawa nilichonacho na nikiangalia humu  ndani (Bungeni) ,wabunge wote mnaonekana  mmepita kwa waganga hawa kama hawapo labda wawili au watatu,kwani Serikali haitoi elimu kwa kundi hili ambalo limekuwa kimbilio la watanzania?" alihoji Kasheku

Akijibu swali hilo, Ummy alisema Serikali inatambua mchango wa watu hao kwa kuwa kundi kubwa linawategemea waganga hao wa tiba mbadala.

Mapema katika swal la msingi Mbunge wa Ushetu Elias Kwandikwa (CCM) alitaka kujua ni waganga wangapi wa kienyeji wamekamatwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kufuatia msako ambao umekuwa ukifanywa na jeshi hilo.

Akijibu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuf Masauni alisema,waganga wa kienyeji waliokamatwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ni 26 na kushitakiwa kutokana na kufanya biashara ya uganga  bila kibali  na kupatikana na nyara za Serikali.

"Katika  kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 jumla ya waganga 16 walikamatwa na kufikishwa mahakamani ,Kati ya hao waganga saba walipatokana na hatia kwa kufungwa miaka miwili kila mmoja au kulipa faini ." alisema Masauni

Alisema,jumla ya watuhumiwa sita katika kesi  tofauti walilima faini ya jumla sh.milioni 1.25, mtuhumiwa wa kesi moja alihukumiwa miaka miwili bila yeye kuwepo mahakamani ambapo juhudi za kumsaka zinaendelea.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo