‘Umeme wa uhakika muhimu kwa viwanda’


Mwandishi Wetu, Mbeya

UCHUMI wa viwanda nchini utawezekana iwapo kutakuwepo na umeme wa uhakika utakaosaidia usindikaji mazao ya kilimo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi kilichoundwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kurudisha uoto wa asili wa Mto Ruaha, Jackson Saitabahu.

Alisema yatawezekana iwapo vyanzo vya maji vitalindwa jambo litakalosaidia hata wakulima wadogo kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao kwa ajili yakuyaongezea thamani.

“Tunatakiwa tuanzishe viwanda vidogo katika maeneo yetu, lakini viwanda vinahitaji umeme na kwani umeshafika vijijini kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA), tutakuwa na umeme wa uhakika, lakini kule umeme unakozalishwa wanategemea maji tunayazungumzia, hivyo muhimu tuyalinde,” alisema Saitabahu na kuongeza:

“Tuna imani kwamba Serikali kuwaletea umeme huku ni haki yenu kwa sababu ndio mnaohifadhi vyanzo vya maji, lakini ili haya yote yakae vizuri inatakiwa maji yabaki vizazi na vizazi kwa kutunza vyanzo vyake.”

Wakiwa katika mfululizo wa ziara Wilaya ya Mbeya mkoani hapa waliagiza mamlaka za ardhi kuweka mipaka kuzunguka vyanzo vya  ili iwe ya kitaalamu na idumu kwa muda mrefu.

Wataalamu hao walitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Inyala wilayani Mbeya mkoani hapa.

Walisema eneo lisilofa kufanyiwa shughuli za kilimo na shughuli nyingine za kibinadamu ni mita 60 kutoka kwenye maji hadi nchi kavu.

Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho Geoffrey Kirenga alisema ipo haja ya kutafuta njia muafaka za kuhifadhi vyanzo vya maji ambazo haziwezi kuathiri shughuli za kila siku za wananchi wa maeneo hayo.

“Tuangalie mbinu na teknolojia ambazo zitasaidia zinatunza maji kuliko hizi tunazotumia sasa, kwa sababu kama mnavyoona maji yanapungua katika vyanzo vyetu kwa kasi kubwa,” alisema Kirenga.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo