Kizimbani akidaiwa kunajisi mtoto


Jemah Makamba

MKAZI wa Kivule, Dar es Salaam, Juma Hassan (40), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akituhumiwa kunajisi mtoto wa miaka 10.

Akisoma mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu John Msafiri, mwendesha mashitaka, Neema Mosha alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 4 Kivule.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, alikana lakini akashindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Juni 3 kesi hiyo itakapotajwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo