JPM kumkabidhi Museveni uenyekiti EAC


Abraham Ntambara

Rais John Magufuli
RAIS John Magufuli leo anatarajia kumkabidhi Rais Yoweri Museveni wa Uganda uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mkutano wa wakuu wa nchi za EAC unaofanyika Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda, Dk Augustine Mahiga alisema hayo juzi alipozungumza na vyombo vya habari, baada ya ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa EAC.

Alisema vikao vya wakuu wa nchi wanachama hufanyika mara mbili kwa mwaka, wakati vingine vikiwamo vya mawaziri hufanyika zaidi ya mara mbili, ili kupima na kutathmini mwelekeo wa ushirikiano wa nchi hizo.

“Katika vikao vya marais huwa na nchi Mwenyekiti, ambaye sasa ni Tanzania, kwa miaka miwili mfululizo, lakini sasa tumemaliza muda wetu na katika kikao hiki cha 18 cha marais, Rais Magufuli atamkabidhi uenyekiti Rais Museveni,” alisema Dk Mahiga.

Alifafanua kuwa kwa mwaka uliopita hadi Aprili, yeye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC na kutokana na muda kwisha, katika mkutano wa mwisho wa mawaziri uliofanyika Arusha, alimkabidhi uenyekiti Waziri wa Uganda.

Kwa mujibu wa Dk Mahiga, ikiwa mwenyekiti wa EAC Tanzania ilifanya mambo kadhaa katika kuboresha uhusiano wa wanajumuiya, ukiwapo ujio wa Sudani Kusini ambayo uanachama wake, ulikamilika chini ya uenyekiti wa Tanzania.

Katika mkutano wa sasa, Dk Mahiga alisema kutakuwa na masuala mbalimbali yatakayozungumzwa na kutolewa uamuzi na marais.

Miongoni mwao ni pamoja na ripoti ya ushirikiano ya miaka miwili iliyopita chini ya uongozi wa Tanzania, ambayo itazingatia sekta muhimu za kiuchumi za biashara, uwekezaji na huduma za kuendesha nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo