Mfumko wa bei wakwaza mjadala bungeni


Suleiman Msuya

WACHUMI wamesema mfumuko wa bei ya vyakula unaolikumba Taifa na nchi nyingine za Afrika Mashariki ni wa mpito na ulisababishwa na ukame ulitokea siku za nyuma. Lakini wakaishauri Serikali ichukue hatua. Aidha, wabunge wamemwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa nafasi kwao kujadili hali hiyo waliyosema ni mbaya.

Wakizungumza jana katika mahojiano na JAMBO LEO, wataalamu hao walisema hakuna sababu ya kufikiria sana jambo hilo wakieleza linaweza kupata ufumbuzi Taifa likiweka mikakati sahihi na kutumia mvua zinazonyesha kwa usahihi.

Mbunge wa Jimbo la Mchinga CUF, Hamidu Bobali alisema Serikali inapaswa  kuruhusu mahindi yaliyo kwenye maghala ya wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa yaingizwe katika soko ili kuwawezesha wananchi kupata chakula kwa bei sawa.

“Pia, tunaomba Spika Job Ndugai atoe nafasi kwa wabunge kujadili hali kwani hali halisi ni mbaya na mimi katika jimbo langu nimeona hali mbaya nadhani kila mbunge atatoa ya moyoni,” alisema Bobali.

Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula alisema wanasubiri bajeti ya Wizara Kilimo Mifugo na Uvuvi ili waone mipango yao ndiPo watajua nini cha kufanya.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU), Profesa Damian Gabagambi alisema kinachoonekana kwa sasa ni tukio la mpito ambalo litatulika baada ya muda mfupi hasa ukizingatia mvua zimeanza kunyesha.

Alisema mvua zinazonyesha zitasaidia kupatika kwa chakula hivyo mfumo huo wa bei za vyakula utadhibitika kwa haraka hivyo wananchi kuhimili gharama za manunuzi.

“Mimi naliona kama suala la mpito kwa sababu vyakula vingi tunavyokula vinatoka shamba moja kwa moja tofauti na wenzetu ambao wanatumia vilivyopo madukani, hivyo mvua zinazonyesha zitatatua tatizo, ila inapotokea kuna kitu kinaingilia uzalishaji wa mazao ni lazima mfumo uongezeke na ukame ni sababu,” alisema.

Alisema chanagmoto ambayo iliikuta Tanzania iligusa katika Ukanda wate wa Afrika Mashariki hivyo ni lazima athari zionekanekane kwa haraka.

Profesa Gabagambi alisema kinachotakiwa ni wizara ya kilimo kupitia kitengo cha usalama wa chakula kujua hali hali ya chakula ili waweze kushauri Serikali kabla hali hiyo haijafikia.

Alisema iwapo kutakuwa na ushirikiano baina ya kitendo hicho na wazalishaji inaweza kuwa njia sahihi ya kutambua upungufu wa chakula na nini kifanyike wakati huo.

Aidha, alisema suala hilo haliwezi kuchukuliwa kisiasa kwani ni dhahiri sababu za msingi zipo kwa hali hiyo kuwepo.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Christopher Awinia alisema sababu ya mfumo wa bei ya vyakula unachangiwa msimu wa kilimo hali ambayo wakulima wengi wanazalisha.

Alisema sababu nyingine inahusu mgogoro ya kivita katika nchi za Burundi na Sudani Kusini hali ambayo inaongeza hitaji la chakula kutokana na kundi hilo kutojihusisha na kilimo.

“Pia miundombinu kuharibika inaweza kuwa sababu ya kukosekana kwa vyakula hasa kipindi hiki cha mvua na pindi kikipatikana bei inakuwa kubwa,” alisema.

Aidha, alisema sera ya kuagiza vitu kutoka nje inaweza kuwa imeaathiri kutokana na kodi ambazo zinakatisha tamaa kwa wafanyabiashara.

Mhadhiri mwandamizi huyo alisema njia ya kusaidia katika maeneo ambayo mfumuko umezidi kuwa mkubwa ni vema Serikali kugawa chakula na kuweka mazingira mazuri ya kuagiza kutoka nje.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwaka uliopita, lakini fahirisi za bei zimeongezeka hadi Sh.109.4 Aprili 2017 kutoka Sh.102 Aprili 2016.

"Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa Machi 2017, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha Aprili imekuwa sawa na Machi 2017,"alisema

Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa Machi.

Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 kwa Machi 2017.

Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 Aprili kutoka asilimia 3.6 kwa Machi.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa dhamani ya shilingi, Kwesigabo alisema  uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh.91.71, Aprili 2017 ikilinganishwa na Sh. 92. 21 ilivyokuwa Machi 2017.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo