Mbunge ahoji ahadi ya Serikali Lushoto


Joyce Kasiki, Dodoma

Shaban Shekilindi
MBUNGE wa Lushoto Shaban Shekilindi (CCM) ameihoji Serikali lini itajenga Chuo cha Ufundi stadi cha Veta wilayani Lushoto ili kutimiza ahadi yake ilivyoahidi kujenga vyuo hivyo katika kila wilaya kwa leongo la kuwasaidia Vijana  nchini kujifunza stadi za kazi mbalimbali .

Akiuliza swali Bungeni jana,Shekilindi alisema,ujenzi wa Chuo katika wilaya ya Lushoto na Nchi nzima kwa ujumla  ,utasaidia Vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

"Je,lini Chuo cha Veta kitajengwa katima wilaya ya Lushoto?" alihoji Shekilindi

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stellah Manyanya alisema,Serikali itaanza ujenzi katika wilaya ya Lushoto mara baada ya kukamilisha miradi ya you ya Veta iliyoanzishwa katika vyuo vya Lidewa,Namtumbo,Chunya na Ukerewe.

Hata hivyo alisema,wakati juhudi mbalimbali zinaendelea za kutafuta fedha na ufadhili wa kujenga vyuo,Serikali  inashauri wananchi wa wilaya ya Lushoto waendelee kutumia Chuo cha Veta cha Mkoa wa Tanga na vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Muheza na Handeni na vyuo vingine vilivyosajiliwa na Mamlaka ya Veta nchini.

Katika swali lake la nyongeza Mbunge huyo alitaka kujua kama Serikali  haioni 
kuchelewa kujenga Chuo hicho wilayani Lushoto ,italimbikiza Vijana wengi watakaoikosa elimu ya veta pia alitaka kujua Kama Waziri yupo tayari kwenda kuwaona baadhi ya majengo yaliyopo wilayani humo ambayo hayatumiki Kama yanaweza kutumika kwa ajili ya kutoa mafunzo ya veta.

Akijibu Mhandisi Manyanya alisema,Serikali haina Lengo la kudidimiza maendeleo ya wilaya ya Lushoto kwa Vijana kukosa elimu ya Veta huku akisema,bado Serikali inaendelea kutafuta fedha na kwamba wakati muafaka ukifika na fedha zitakapopatikana,Serikali itajenga Chuo hicho.

Aidha alisema,ataenda wilayani Lushoto kuwaona majengo hayo na kama ataona yanafaa,Setikali itayatumia kwa ajili ya kuanzisha Chuo cha Veta.

Alitumia fursa hiyo kuiomba  Serikali  kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupeleka msaada wa haraka ili kurejesha mawasiliano ya barabara ya Lushoto-Dar es Salaam kufuatia kubomoka kwa madaraja katika barabara hiyo.

Shekilindi alitoa kauli hiyo Bungeni mjini hapa jana wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza ambapo alisema, mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Lushoto mkoani Tanga zimeleta madhara na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano katika barabara ya Lushoto-Dae Es Salaam, Lushoto-Arusha na Lushoto-Tanga jambo ambalo limeathiri uchumi wa wakazi wa wilaya hiyo.

Alisema mvua hizo zimesababisha madaraja kukatika na kwamba zaidi ya kilometa 32 katika barabara hiyo hazina mawasiliano,huku akisema  msaada huo utasaidia kunusuru maisha ya wananchi wa Lushoto na uchumi unaotegemea barabara hiyo.

“Mheshimiwa naibu spika kwa kuwa jambo hilo ni kubwa na limeathiri uchumi wa wakazi wa Lushoto niambe serikali ipeleke msaada wa haraka, pia nitoe pole kwa wananchi wa jimbo la Lushoto na wilaya ya Lushoto kwa ujumla,”alisema.
Shekilindi alibainisha kuwa, tarayi alikwisha zungumza na Menea wa  Wakala wa Barabara(TANROAD), mkoa wa Tanga ambaye aliahidi kushugulikia jambo hilo, anaamini kuwa litashughulikiwa haraka.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo