KKKT yatenga Sh milioni 40 kusomesha wafugaji


Mery Kitosio, Meru

KANISA la KKKT, Dayosisi ya Meru imejiwekea utaratibu wa kutumia Sh. milioni 40 kwa mwaka kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi wanaotokea familia zisizo na uwezo pamoja na watoto wa kike wanaotokea kabila la Kimasai ambao wanaozeshwa kwa nguvu.

Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo Elias Kitoi alipokuwa akizungumza katika sherehe za mahafali ya sita ya kidato cha sita ya Seminari ya Ailanga.

Askofu Kitoi alisema kuwa wamekuwa wakitafuta wale watoto wa masikini ambao wanatokea shule zote  zilizopo ndani ya eneo la meru na hata watoto wa kike ambao mara nyingi wamekuwa wakikosa elimu kwa ajili ya kuozeshwa kwa nguvu kwa kuwasomesha hadi kilele wanachopenda ili kuwawezesha kutimiza malengo ya elimu kama zilivyo jamii nyingine.

"Tulishawasaidia wanafunzi wengi sana kwa utaratibu huu kwani sisi tunaangalia tu wale wanafunzi ambao wanafanya vizuri katika mitihani ya mwisho ya kidato cha nne na sita  na kuamua kuwaendeleza hadi chuo kikuu kwa kuwafadhili sisi pamoja na wafadhili kutoka nchi za nje ambao nao waliupenda sana huu utaratibu wetu,"aliongeza Askofu Kitoi.

Alisema mbali na kuwasaidia watoto hao wamekuwa pia wakitoa kipaumbele sana sehemu ambazo hadi sasa elimu haithaminiwi  kama sehemu za umasaini ambapo kumeoneka kuwa elimu kwa watotot wa kike haipewi kipaumbele na hivyo kufanya maeneo hayo kubaki nyuma kimaendeleo.

Awali, mkuu wa seminari hiyo Wilium Lowasa aliiomba Serikali kutupia jicho la pili upatikanaji wa maji safi na salama shuleni hapo kwani yaliyopo kwa sasa yana kiwango kikubwa cha floride hivyo kuufanya shule kutumia gharama kubwa mno kwa ajili ya utafutaji wa maji safi kwa usafiri wa gari.

Aidha alidai kuwa kwa sasa shule hiyo imejiwekea mikakati ya kuhakiisha inakuwa ya kwanzz kitaifa kwa kubadilisha mfumo wa mitihani ambapo kwa sasa wamekuwa wakitunga mitihani iliyo sawa na kitaifa ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kupambana na mitihani yao ya mwisho.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo