Wabunge EALA waepuke ‘siasa za ndani’, waiangalie


Mashaka Mgeta

Mashaka Mgeta
NI dhahiri kwamba uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa upande wa upinzani katika Tanzania, ulizongwa na hisia za ‘mizengwe’, matakwa ya siasa za ndani ya nchi na kukomoana.

Lakini wapo walioamini kwamba upinzani, hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hakikutumia uwiano wa jinsia kuwasilisha majina ya wagombea wake katika hatua ya awali iliyowahusisha Ezekiel Wenje na Lawrence Masha.

Wawili hao waliteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa EALA, lakini kura zao hazikutosha, hivyo Bunge (ingawa kwa kushutumiwa kutumika kwa maslahi ya kisiasa) lilikiamuru chama hicho kuwasilisha majina ya wagombea kwa awamu ya pili.

Chadema ikawasilisha majina ya Profesa Abdallah Safari, Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha na Pamela Massay. Miongoni mwao, Lamoyan na Maassay walishinda.

Zipo hekaya nyingi zinazoenea kuhusu kukataliwa kwa Wenje na Masha, nyingine zikielekezwa katika hofu kwamba kupitia ubunge huo, wawili hao wangeimarisha nguvu za upinzani katika ukanda wa Ziwa Victoria. Inasemwa hivyo.

Wapo wanaoamini wana uzoefu katika masuala ya kikanda na kimataifa, Wenje alikuwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati Masha alifikia hatua ya kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa nyadhifa hizo, wawili hao walitarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi kupitia EALA, lakini walikataliwa kwa awamu mbili na wabunge. Lakini iwe iwavyo, Wenje na Masha hawataingia EALA wakitokea upinzani hususani Chadema, bali Lamoyan na Maassay watakaoungana na Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahaya, Dk Abdallah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Alhaj Adam Kimbisa (wote kupitia CCM) na Habibu Mnyaa (CUF).

Pamoja na hali ilivyokuwa katika kuwapata wabunge hao, sasa nchi inapaswa kuwa katika ‘umoja timilifu’ inapojielekeza katika maslahi yake kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Tanzania haipaswi kuziibua tofauti za siasa za ndani zijikite katika EALA. Itakuwa ni kujiangamiza.

Ikumbukwe kwamba EAC ni jumuiya yenye nchi sita zilizo wanachama, zikiwamo waasisi wake Tanzaia, Kenya na Uganda zilizosaini makubaliano ya kuanzishwa kwake Novemba 3, 1999 na utekelezaji wake kuanza rasmi Julai, 7, 2000.

Nchi nyingine ni Rwanda na Burundi zilizosaini mkataba huo Juni 18, 2007 na kuwa wanachama kamili kuanzia Julai, Mosi, 2007. Sudan Kusini iliyo mwanachama mpya ilisaini mkataba huo Aprili, 15 mwaka jana na kuwa mwanachama kamili Agosti, 15 mwaka jana.

Ni jumuiya yenye watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 150, miongoni mwao asilimia 22 pekee wakiwa wanaishi maeneo ya mijini, hivyo kuifanya asilimia kubwa (asilimia 78) kuishi vijijini, wengi wao wakijishughulisha na kilimo na ufugaji. Hivyo kuwa katika EALA si suala la ‘lelemama’, si fursa ya kuendeleza u-CCM, u- Chadema ama u-CUF.

EALA ni jukwaa lenye kusimamia kwa dhati maslahi ya nchi ndani ya mkataba uliosainiwa na kuzishirikisha nchi sita. Itakuwa fedheha na Tanzania itachekwa na dunia ikiwa wabunge waliochaguliwa kuingia EALA watajikita katika tofauti zinazotokana na siasa za ndani, wakiwaacha wabunge wenzao wakizitetea nchi zao na maslahi yanayogusa maisha ya watu wao. Ijulikane kwamba pamoja na kuwa na Jumuiya ya kikanda, kila nchi inabaki kuwa na maslahi yake binafsi yanayoweza kuathirika kupitia uamuzi unaochukuliwa baada ya mijadala inayofanyika ndani ya EALA.

Kwa maana EAC ni ukanda unaochochea ushirikiano na muingiliano katika maeneo tofauti kwa maslahi ya kila upande. Maeneo hayo ni pamoja na siasa, uchumi na jamii.

Kwa sasa, ushirikiano wa kikanda unaendelea vema katika masuala ya ushuru wa forodha, uanzishwaji wa soko la pamoja na utekelezaji wa itifaki ya sarafu moja katika ukanda huo.

Lakini yapo masuala mengi kuanzia KWA Ujinga Wangu nimejaribu kuangalia utendaji wa baadhi ya viongozi wa zama hizi na zilizopita na kubaini kuna tofauti kubwa ya utendaji wa kazi.

Ninasema hivyo kwa sababu kwa umri nilionao nimeona awamu nyingi za uongozi ndani ya nchi yetu na namna walivyofanya shughuli zao. Zama zile waliamini kwenye kutumikia wananchi kutoka moyoni na walifanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Tena wakati huo wala hakukua na vyombo vingi vya habari kama ilivyo sasa. Walikuwa na njia ambazo walitumia kuwasaliana na wananchi wao katika masuala mbalimbali ya maendeleo. Ilikuwa ni nadra kuwaona wakikimbilia kwenye vyombo vya habari kujieleza walichofanya.

Utendaji wao ulijionesha wazi kwa wananchi kwa namna walivyosimamia majukumu yao. Sikuona iwe mkuu wa mkoa wa mkuu ama wilaya wakitumia vyombo vya habari mara kwa mara ili kuonesha waliyoyafanya.

Kwa Ujinga Wangu hii ni kwa sababu waliamini utendaji kazi unaweza kujulikana kwa wananchi bila hata kutumia chombo cha habari. Viongozi waliopita waliamini utendaji kazi wao unaonekana moja kwa moja kwa wananchi na si kutumia vyombo hivyo kujitafutia umaarufu.

Nimeamua kujadili mada hii baada ya kuona baadhi ya viongozi wanatumia muda mwingi na nguvu kubwa kutafuta fursa ya kuzungumza kwenye vyombo vya habari badala ya kutumia nafasi waliyonayo kushughulikia matatizo ya watu.

Kwa Ujinga Wangu kwa kusema hivyo sina maana kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine serikalini wasitumie vyombo vya habari, hapana bali wavitumie kwenye mambo ya msingi ambayo umma lazima ujulishwe.

Nafahamu chombo cha habari kinarahisisha kufikisha ujumbe wa kiongozi kwa wananchi wake kwa haraka zaidi na hivyo lazima vitumike lakini si kwa kila jambo.

Siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya wakuu wa mikoa kuona chombo cha habari ndiyo kimbilio lake.

Asipoonekana kwenye runinga anahisi anaumwa na yupo tayari ku-ACHA NIPAYUKE Mashaka Mgeta ngazi za kitaifa hadi zile za msingi zinazowagusa wananchi wa kawaida walio walengwa wakuu katika ushirikiano huo.

Uhusiano wa raia wa mataifa hayo upo katika maeneo yenye tija na faraja, lakini pia katika mizozo inayoweza kuhatarisha usalama, mali na maisha ya watu.

Hayo ni baadhi ya mambo machache kati ya mengi ambayo wabunge wa EALA kutoka Tanzania wanapaswa kuyatilia mkazo, kuyajua kwa kina na kuyahusisha na misimamo katika sera za nje za nchi, ili kila watakapotimiza wajibu wao, waiweke Tanzania na Watanzania mbele ya vyama vyao.

Itakuwa ni kuukwepa ukweli kwamba hisia za kuwa ‘mizengwe’ katika uchaguzi wa mwaka huu hususani katika kambi ya upinzani, hazipaswi kupuuzwa. Madhara yanayoweza kutokana na matokeo ya ‘mizengwe’ hiyo hayataviathiri vyama vya siasa bali Tanzania na Watanzania.

Lakini kama walivyosema wahenga, maji ukiyavulia nguo, hauna budi kuyakoga. Sasa wabunge waliobainika kuwa wenye maslahi kwa nchi kupitia kwa wawakilishi wa wananchi, wameshachaguliwa kuingia katika EALA.

Jambo la msingi ni kutoziendekeza siasa za ndani na tofauti. Kama uchaguzi huo, pamoja na ‘mizengwe’ inayotajwa ulikuwa wenye heri basi heri hiyo iendelee kuwapo, lakini ikiwa itaibua shari, basi Watanzania waungane kuliepusha Taifa na shari zote, ushindi utakuwa kwa wote.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo