Sumatra yaitisha kikao na wadau


Venance Matinya, Mbeya 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) imefanya mkutano na wadau wa usafirishaji mkoani Mbeya wenye lengo la kupokea maoni ya kurekebisha na kuboresha kanuni mbalimbali. 

Akifungua mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa, Mwenyekiti wa Mkutano ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani, Henry Bantu alisema lengo ni kushirikisha wadau kwenye mchakato huo. 

Alisema kanuni zinazopitiwa ni pamoja na kanuni za Leseni za usafiri wa magari ya abiria, 2017, Marekebisho ya kanuni za leseni za usafirishaji wa pikipiki 2017 na Marekebisho ya kanuni za leseni za usafirishaji wa Magari ya mizigo ya mwaka 2017. 

Alisema sekta ya usafiri ni muhimu katika Serikaliya awamu ya tano katika kuelekea kwenye Nchi ya Uchumi wa Viwanda hivyo ili kupata mafanikio ni bora kuboresha sekta hiyo. 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Sheria Sumatra makao makuu, Leticia Mutaki alisema lengo la maboresho ya kanuni hizo ni kuhakikisha usafiri wa barabara unakuwa bora na salama, viwango vya adhabu vilivyopo vinaendana na wakati na kuendana na mabadiliko ya usafiri wa barabara. 

Alitaja malengo mengine kuwa ni kuendana na mikataba ya kimataifa pamoja na kuongezeka kwa huduma za usafiri mbalimbali ambazo zilikuwa hazimo kwenye kanuni. 

Kwa upande wake mmoja wa Wadau wa Usafiri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri
(CCC)Sumatra Mkoa wa Mbeya, Said Mohamed alisema tatizo sio mapungufu ya Kanuni bali ni changamoto ya usimamizi kutoka Sumamtra. 

Alisema mara nyingi abiria hupoteza mizigo kwenye magari lakini hakuna hatua zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa tiketi ambazo haziendani na kanuni za usafirishaji kwani baadhi huandika mizigo sio dhamana ya msafirishaji. 

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni ubovu wa magari yanayopewa leseni ya kusafirisha abiria kutokana na muundo wa ukaguzi  ambao hufanywa na Polisi lakini Sumatra anatakiwa kutoa kibali bila kujiridhisha.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo