Kesi ya waliofutiwa udahili Juni 29


Grace Gurisha

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kusikiliza kesi ya madai iliyofunguliwa na wanafunzi 316 waliofukuzwa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kwa madai ya kutokuwa na sifa za kudahiliwa kwenye vyuo vikuu nchini, wakidai fidia ya Sh. bilioni sita, Juni 29 mwaka huu.

Kesi hiyo itasikilizwa mbele ya Jaji Wilfred Ndyansobera, baada ya pande zote kushindwa kumaliza kesi hiyo nje ya Mahakama. Wanafunzi hao wamefungua kesi hiyo dhidi ya chuo hicho na Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Wanafunzi hao walifungua kesi hiyo namba 122 mahakamani hapo kupitia wakili wao Emmanuele Muga. Wanafunzi hao wanadai Sh.bilioni moja kwa ajili ya mjumuisho wa ada na vifaa tangu wakae chuoni hapo, huku Sh.bilioni tano kama fidia.

Katika madai hayo walieleza kuwa TCU iliwaruhusu kudahili wanafunzi wa Shahada ya Sayansi kwa miaka mitano, huku miaka miwili ikiwa kwa ajili ya kusafisha cheti cha kidato cha nne na miaka mitatu iliyobaki kwa ajili ya kusomea Shahada.

Wamedai kuwa baada ya TCU kutoa tamko Mei mwaka jana  kwamba wanafunzi hao hawana sifa walirudi nyumbani, huku miongoni mwao wakiwa tayari wamesoma kwa miaka mitatu, miwili na mmoja.

Wanafunzi hao wamedai kuwa awali wakiingia chuoni hapo walilipa karo iliyojumuhisha na vifaa vya chuo kwa Sh.milioni moja kwa kila mwanafunzi. Awali mahakama hiyo ilikubali kutoa kibali cha kufungau kesi ya uwakilishi kwa wanafunzi 316, ambao watawakilishwa na  Ramadhan Kipenya, Innocent Peter, Oswald Mwinuka na Feith Kyando.

Hivyo kutokana na kufukuzwa chuoni hapo, wameiomba mahakama iiamuru TCU na chuo cha Mtakatifu Joseph kuwalipa kiasi hicho cha Sh.bilioni moja kwa ajili ya wanafunzi wote na Sh.bilioni tano kama fidia.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo