RC Gambo akabidhiwa rambirambi maafa ya Lucky Vicent


Mery Kitosio na Wankyo Gati, Arusha

Mrisho Gambo
TAASISI za Eco valley advisers, Clouds media pamoja na Time tickets, wamekabidhi kwa uongozi wa mkoa wa Arusha Sh 4,444,0331, ikiwa ni rambirambi zilizochangwa na Watanzania kupitia mfumo wa harambee wa kusaidia janga la ajali lililotokea katika shule ya luck vicent.

Rambirambi hiyo ilikabidhiwa jana kwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kushuhudia na uongozi wa shule hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, mshauri elekezi wa Time ticket Avit Buchwa alisema kuwa taasisi hizo zilikubali kwa pamoja kuunganisha nguvu katika kusaidia kwa hali na mali pindi mtu au kikundi kinapopata majanga.

Alisema kuwa ndani ya kipindi kifupi kichozidi siku nne wachangiaji wapatao 721 waliweza kuchangia kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza kwa niaba ya wafiwa na wakazi wa Arusha, mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo alisema kuwa amefarijika sana kuona Watanzania wakiwa wamoja katika kipindi hiki cha majonzi.

Gambo alisema kuwa ni jambo la kutia moyo na kujivunia kwamba sasa upo mfumo wa harambee wa tehama ambao unaweza kukusanya michango kwa ufanisi na uwazi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo