Kesi ya Scorpion yaahirishwa tena


Jemah Makamba

KESI inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’, ya kuiba, kujeruhi na  kumtoboa macho Saidi Mrisho, imehairishwa tena  na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kutokana na Wakili wa mlalamikaji kukosekana mahakamani.

Mashitaka hayo yaliahirishwa kwa maombi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na Hakimu Flora Haule huku Wakili akidai  kuwa upande wa Jamhuri imeandaa shahidi mmoja wa tisa.

"Shauri lilikuja kusikilizwa upande wa Jamhuri tulijiandaa na shahidi mmoja, lakini tunaomba tarehe nyingine kutokana na Wakili wa mshitakiwa kutokuwapo mahakamani," aliomba Katuga.

Hakimu Haule alikubali maombi hayo na kupanga Juni 8 kuwa siku ambayo kesi hiyo itatajwa na kutolewa siku ya kusikilizwa, huku mshitakiwa akirudishwa rumande.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo