Kituo cha Uwekezaji chapata bosi


Mwandishi Wetu

RAIS John Magufuli amemteua Geoffrey Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), huku aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, akiteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Kabla ya uteuzi huo, Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Singida.

Taarifa ya Ikulu Dar es Salaam jana ilieleza kuwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.

Kwa mujibu wa tarifa hiyo, Rais Magufuli alimteua Clifford Tandari aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, akichukua nafasi ya Dk John Ndunguru ambaye amestaafu.

Tandari alikuwa anakaimu nafasi hiyo TIC, baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wake, Juliet Kairuki Aprili mwaka jana, baada ya kubainika hajapokea mshahara wake tangu alipoajiriwa mwaka 2013.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo