KACU yatishia kugomea ushuru


Shaban Njia, Kahama

Matomora Michael
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Ushetu Wilayani hapa, Matomora Michael, amesema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika (KACU), wametishia kutotoa ushuru wa asilimia tano kwa halmashauri hiyo kwa kile kinachadaiwa kuwa fedha hiyo hairudi katika maeneo ya wakulima wa tumbaku kwa ajili kutengeneza miundombinu ya barabara. 

Matomora aliyasema hayo juzi katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika kata ya Nyamilangano ambapo alisema kuwa kitendo cha chama cha ushirika kutishia kutoa ushuru wa zao la tumbaku ni kwenye kinyume na makubaliano ya ulipwaji kodi serikalini. 

Alisema usemi huo ni upotoshaji kwa wakulima wazao la Tumbaku ambalo ushuru wao mkubwa ndio inaotegemewa na Halmashauri hiyo kama mapato ya ndani na kuongeza  kuwa barabara hizo tayari zimtengenezwa kwa kiasi kikubwa  katika maeneo makubwa ambayo kimsingi ndio yanayolima zao la Tumbaku kwa kiasi kikubwa. 

Aidhaa alisema ushuru kwa Halmashauri hiyo sio kwa ajili ya kutengeneza barabara tuu na kuongeza unaweza kutumika katika mambo mengine ya msingi yenye maslahi na Halmashauri hiyo ili kuhakikisha kuwa maendeleo yanapatikana na Wananchi wanapata huduma zinazotakiwa za kijamii. 

“Fedha hizo zinazotolewa na Chama kikuu cha Ushirika Wilayani Kahama sio kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya Barabara tuu katika Halmashauri yetu bali zinaweza kutumika katika kufanya kazi zingine zenye maslahi na Halmashauri yetu ili kuwaletea wananchi maendeleo katika eneo husik”, Alsema Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Ushetu. 

Katika hatua nyingine Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga juzi ililaani vikali na kukanusha rasmi kuhusi kitendo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli kutangaza katika Vyombo ya habari kuwa ametoa msaada wa ujenzi wa barabara ipatayao mitaa 200 katika eneo la Kata Bulungwa Wilayani hapa 

Akiongea katika kika kikao cha baraza Madiwani juzi kiklichakaa katika makao makuu ya Halmashauri ya Ushetu Nyamilangano, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Matomora Michael alisema kuwa kitendo alichokisema Mbunge huyo katika vyombo vya habari ni kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Alisema Kuwa Halmashauri yake ya Ushetu ina kila kumbukumbu ya Mtui yryote ambaye anakuwa akitoa msaada na kuongeza kuwa katika ofisi yake hajaona faili lololeau taarifa inayisema Mbunge huyo ametoa msaada wa kujenga barabra katika kata ya Bulungwa ya kiasi cha mita 200. 

“Mimi ninashangaa kwa James Lembeli lusema kuwa ametoa msaada wa ujezi wa barabara ya mita 200 katika eneo amblo lipo kariu na mahali anapoishi huku kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini hajawahi kujenga hata kilometa moja leo hayupo katika wadhifa huo atawezaje kujenga”, Alisema Matomora 

Aliendelea kusema kuwa kauli hizo zinaotolewa na  Lembeli ni katika hali ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuongeza barabara hiyo ambayo inatoka katika kata ya Bulungwa kwenda katika Vijiji vya Karo na Nyankende wananchi ndio walitoa mafuta kwa ajili ya utengenezwaji wa kipande hicho na kuongeza lembeli yeye alishirikishwa kama mkazi wa eneo hilo. 

“Sisi kama Halmashauri ya Ushetu tunashangaa Mungunge huyo aliyeongoza jimbo hilo hilo liliokuwa Kahama Mjini hapo awali  kuwa barabara ya kilometa tisa  yeye anatafuta umaarufu  kwa mita 200 tuu huku Halmashauri yetu ikiwa haina kumbukumbu yeyote ya mtu ambaye anaamua kujitilea kufanya jambo fulani lamaenedeleo katika eneo husika”, Aliongeza Matomora.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo