Wauguzi Pwani wadai hawana vitendea kazi


Mwandishi Wetu

WAUGUZI katika Mkoa wa Pwani wamelalamikia kukosa sare za kazi, hivyo kulazimika kujinunulia wenyewe, baada ya mamlaka kushindwa kuwapa fedha za kununua.

Hayo yalielezwa na mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi mkoani humo, Elias Bulole alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema licha ya mafanikio wanayopata kazini, ikiwamo kuinua huduma za afya, kutopewa fedha kwa ajili ya kununua za sare za kazi ni moja ya changamoto zinazowakabili.

“Pia tunakabiliwa na upungufu wa dawa na vitendea kazi bora katika vituo vya kutolea huduma,” alisema Bulole.

Mwenyekiti huyo pia alitaja ukosefu wa nyumba za karibu na maeneo ya kazi, wauguzi wanaojiunga na masomo ya kujiendeleza kutolipiwa ada na kuchelewa kupandishwa vyeo kuwa ni changamoto zingine  zinazowakabili.  

Pia alitaja kutokuwepo kwa maji katika vituo vya afya na zahanati kuwa ni kero inayowafanya wauguzi kufanya kazi katika mazingira magumu.

Alisema katika idara ya afya mkoani Pwani asilimia 80 ya  kazi za afya zinafanywa na wauguzi na kwamba kwa sababu hiyo ni vyema wakapewa kipaumbele katika mambo mbalimbali.

“Tupewa elimu ya kutosha, mazingira mazuri ya kazi sanjari na uongezaji wa wauguzi kutoka ni 891 tuliopo sasa hadi 2,591wanaohitajika,” alisema Bulole.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happiness Seneda alikiri kuwepo changamoto hizo na kuahidi kuwa serikali ya wilaya itajitahidi kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.

Seneda alisema wauguzi wote wanafanya kazi ya Mungu hivyoo ni vyema wakaendeleza tabia ya unyenyekevu kwa wagonjwa.

Katibu wa Afya mkoa wa Pwani Alfred Karaba alisema changamoto za wauguzi zinajulikana lakini mafungu yanayotoka serikalini bado hayatoshelezi ambapo alishauri kila halmashauri kuzitatua kulingana na mafungu wanayopewa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo