Zitto amchachafya Prof Mkenda kuhusu viwanda


Joyce Kasiki, Dodoma

Zitto Kabwe
MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) ametishia kurudisha shahada aliyonayo kwa mwalimu wake, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, iwapo mwalimu huyo atashindwa kuisimamia vizuri wizara hiyo.

Akichangia katika hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018   ya Zitto alisema ana imani Profesa Mkenda   ataitendea haki wizara hiyo. 

“Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu wako ni mwalimu wangu wa uchumi, mwaka wa tatu ameniundisha sekta zote za uchumi yaani unachukua unatafuta njia hii na njia hii ukiingiza unapata kila kitu. Mimi sitaki kumwambia nimrudishie Digrii yake kwa sababu kwa sasa yeye ndio Katibu Mkuu katika wizara hivyo anawajibika,” alisema.

Zitto ameitaka Serikali kuhakikisha inafanya kila jitihada katika kuendeleza zao la katani  akisema: "Hivi Mheshimiwa Mwijage mnakaa katika ‘Cabinet’ mnajadili  hii mipango kwa sababu mkikaa lazima kuna mtu atasema mimi  kuna miradi yangu,lakini tunajenga mabehewa,mabehewa yana viti ,hivi mmefikiria namna gani ya kuendeleza zao la katani.’’

 Aliongeza: "Leo tunakutana baada ya mwaka mmoja ukichukua Mwezi Marchi 2016 na Mwezi Marchi 2017 bidhaa za Viwanda ambazo tunauza nje zimeshuka kwa dola za Kimarekani milioni 500 kutoka 1.4 mpaka 0.9 milioni dola sasa. Tunaposimama hapa na kusema kazi inafanyika ,Waziri atusaidie kwamba iwapo kazi inafanyika na  kuna ongezeko la uzalishaji ni kwanini mauzo yetu nje yamepungua kwa kiwango kikubwa.’’

Alisema,mambo hayo wabunge wanapaswa kuyazingatia  kwa sababu bidhaa za viwanda zinazouzwa nje zinapopungua ,ni kwamba Viwanda vyetu vya ndani vimepunguza uzalishaji maana kuna watu wamepoteza kazi maana kuna mapato ya serikali yanapotea’’ alisema

Zitto alisema, ndani ya miezi 12 ,Tanzania imepoteza  mauzo nje kwa dola milioni 500 ambapo alidai ifikapo mwaka  2020   inawezekana kabisa kusiwe na hata senti moja kutokana na mauzo ya nje.

Alisema, Tanzania ina tatizo kubwa la kulinda viwanda vya ndani ambapo alidai Waziri wa Wizara hiyo ni shahidi juu ya malalamiko anayopelekewa kila mwisho wa mwezi ya watu ambao wanaingiz nguo kinyemela nchini.

‘’Wanaingiza mafuta ya kula kinyemela katika nchi yetu,wanaingiza Betri zinakuwa za bei ndogo na matokeo yake ni kwamba Viwanda vya ndani vinashindwa kushindana nao katika soko’’

Alihoji ,takwimu za kiwango gani cha betri Tanzania imeagiza kutoka China miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016 kwani ukienda Idara ya wateja ya China utakuta kwamba, kati ya Januari mpaka Septemba mwaka jana Tanzania imeingiza  Betri za China zenye thamani ya Dola za Kimarekani  36.5.

"Ukija kuangalia kwa Idara yetu ya Forodha hapa nchini betri ambazo zimeingia nchini na ukalinganisha na TBS betri ambazo wamezifanyia ukaguzi kuwa ngapi zimeingia nchini ni za dola Kimarekani milioni 5.3 maana yake ni kwamba kuna betri nyingi sana ambazo zinaingia nchini hazipiti katika njia ya kawaida’’

Alisema Viwanda ambavyo vinazalisha betri hapa nchini kama Panasonic ambavyo vimeajiri watu vitakuwa vinashindwa kushindana na vile vya China.

"Tafsiri yake ni kwamba tutaongea humu kuhusu viwanda na haya ni mambo ambayo tunategemea kuona Waziri ukihangaika nayo kwa sababu Wahenga wanasema bora ndege ambaye unayemkononi kuliko ambaye yupo juu ya Mti

"Tuna mradi wa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 7 katika reli,reli material yake sehemu kubwa ni chuma unahitaji tani 50 za Chuma cha pua kujenga Kilomita moja ya reli sio kwamba hatuna chuma tunacho Mchuchuma na Liganga’’

Alisema,kabla ya kuanza kufikiria kutandika hayo machuma ya reli ilitakiwa Serikali iwe imeshajenga uwezo  wa kuzalisha kule ili fedha zote zibaki kule na ndani ya nchi .

Aidha, Zitto ambaye pia ni kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo ,aliitaka Wizara hiyo kushughulikia miradi inayotengeneza ajira za ndani ambazo zingesaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea ukuaji wa sekta ya Viwanda huku akitolea mfano wa reli.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo