JPM kukabidhiwa taarifa ya mchanga leo


Hussein Ndubikile

Rais Magufuli
RAIS John Magufuli leo anatarajia kupokea taarifa ya Kamati Maalumu ya Kuchunguza Mchanga mchanga wenye madini.  

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya wajumbe wanane aliyoiunda  Machi kumaliza kazi yake.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Profesa Abdulkarim Mruma, Profesa Justianian Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk Yusuf Ngenya, Dk Joseph Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery Gombela.

Kamati hiyo iliongozwa na Profesa Mruma ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa tukio la upokeaji taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali huku likitarajiwa kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari na tovuti rasmi ya Ikulu.

Msigwa alisema matangazo ya kupokea taarifa hiyo yataanza kurushwa mbashara kuanzia saa 3:30 asubuhi kutoka Ikulu huku ikiwasisitiza wananchi kutazama na kusikiliza.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo