Majeruhi ajali ya Arusha kutibiwa Marekani


Mery Kitosio, Arusha

Mrisho Gambo
MAJERUHI wa ajali  ya gari iliyohusisha vifo 35 vya wanafunzi, walimu pamoja na dereva wa shule ya msingi Luck Vicent  wilayani Karatu, wamesafirishwa jana kwenda Marekani kwa ajili  ya matibabu zaidi .

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Kia, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa majeruhi hao wanasafirishwa na ndege ya Shirika la Samaritan Purse ili kuwawezesha kupatiwa huduma za matibabu zaidi ambazo zitaweza kurejeshea afya zao.

Gambo alisema kuwa Serikali imejitahidi kwa hali  na mali kuhakikisha kuwa wamewafariji wale wote waliofikwa na msiba na hata kuhakikisha kuwa majeruhi waliobaki wanapatiwa huduma ambazo zitaweza kunusuru maisha  yao.

Gambo aliwataka wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwa inakwamisha huduma za kijamii kwa ajili ya kuchanganya na shuguli za kisiasa.

"Naombeni sana wana Arusha muache kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwani hii mitandao imepotosha sana mambo mengi imehusisha huduma za kijamii kuwa mambo ya kisiasa hali ambayo inasababisha hata wanaojitokeza kuchangia maafa haya kuvunjika moyo kwa ajili ya mambo yaliyoandikwa kwenye mitandao ya hiyo"-alisema Gambo

Alidai kuwa huduma za kijamii hazipaswi kuhusishwa na shughuli za kisiasa kwani endapo zitahusishwa zitakwamisha hata wale wanaoendelea kufariji kushindwa kuendelea na moyo huo.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye ni mmoja wa waliojitolea kufanikisha safari hiyo aliwataka Watanzania kuendelea kuombea majeruhi hao ili wapone haraka.

Safari ya majeruhi hao kuelekea Marekani saa 5:40 asubuhi wakiambatana na mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Gaspa ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadiki.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo