Said Mwishehe
Profesa Joyce Ndalichako |
SERIKALI imetatua changamoto ya vifaa
vya kufundishia masomo ya Sayansi katika sekondari za kata baada ya kuingiza kontena
17 za vifaa vyenye thamani ya Sh bilioni 16.9. Vifaa hivyo vitaanza kusambazwa
leo kwenye sekondari hizo na chini ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza jana Dar es Salaam wakati
akipokea vifaa hivyo, Kaimu Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Nicolas Buretta, alisema anaamini wanafunzi watajifunza
Sayansi kwa vitendo, kwani vifaa hivyo ni vya kutosha.
“Wizara tumepokea vifaa vya
kufundishia masomo ya Sayansi kutoka kampuni ya Lab Equip Ltd ambayo ilishinda zabuni
hii.
“Pia tumewaomba JWTZ kuvisambaza
kwenye sekondari zote za kata zilizokamilisha maabara. Tunatarajia usambazaji huu
utakamilika mwezi huu,” alisema Buretta.
Alifafanua kuwa changamoto ya uhaba wa
vifaa vya kufundishia masomo ya Sayansi imekuwa ya muda mrefu, lakini sasa
imefika mwisho baada ya kuanza kuwasili kwa kontena 17 za vifaa hivyo.
Wakati huo huo, alisema ili
kukabiliana na uhaba wa walimu wa Sayansi, Wizara imeomba kibali cha kuajiri
walimu 3,104 ili kupunguza uhaba huo.
Alisema lengo ni walimu 4,129 lakini
waliamua kujiridhisha kwa sifa za walimu hao na kufanikiwa kupata walimu 3,104
wenye sifa stahiki na ndio watakaoajiriwa.
0 comments:
Post a Comment