Dalila Sharif
ULAJI ovyo
wa vyakula visivyofaa husababisha ongezeko la uzito wa mwili (unene) na vitambi
hali ambayo huweza kusababisha magonjwa kisukari, moyo, shinikizo la damu na hata
saratani.
Hayo
yalisemwa Dar es Salaam jana na Ofisa Lishe wa Taasisi ya Lishe na Chakula
Tanzania, Julieth Shine, akisisitiza kuwa ulaji wa vyakula usiofaa husababisha
watu kuota vitambi hasa vyakula vyenye mafuta.
Alisema ulaji
wa vyakula usiotarajiwa husababisha unene uliopitiliza na kusababisha watu
kuzidiwa na uzito wa miili uliopitiliza.
“Hali
hii inatokana na kukosa mtindo bora wa maisha, matumizi ya teknolojia ambayo yamefanya
watu kutumia mashine kufanya kazi za nyumbani badala ya miili hivyo kukosa
mazoezi,” alisema Shine.
“Ni vema
kuzingatia mazoezi na kula kwa wakati kwa usiku mtu kula saa mbili na hivyo kusaidia
kupunguza unene,” alisema Shine.
Alisema
taasisi ina mipango ya kutoa elimu juu ya lishe na kuendeleza mkakati wa Taifa wa kuzuia
lishe isiyofaa.
0 comments:
Post a Comment