Magendela Hamis
Salum Mayanga |
WAKATI timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ikianza
kambi jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga, amesema mshambuliaji Thomas
Ulimwengu kutoka AFC Eskilstuna ya Sweden hatoweza kujiunga na wenzake kutokana
na kuwa majeruhi.
Taarifa ambazo Mayanga amezipata kutoka Sweden ni kwamba
Ulimwengu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo ya AFC Eskilstuna.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari
Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Mayanga atabaki na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk-Ubelgiji), Ibrahim
Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu
Shooting).
Mbali ya hao, nyota wengine aliowataja Jumatatu iliyopita
ni walinda milango, Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na
Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja
Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto
wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga
SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC)
ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude
(Simba SC).
Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam
FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba)
wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya
(Simba SC).
Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na
Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati wasaidizi wake ni Kocha wa Makipa, Patrick
Mwangata, Meneja wa timu, Danny Msangi, Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari
wa timu ni Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25,
2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati
huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
0 comments:
Post a Comment