Ibrahim Kunoga, Tanga
SERIKALI imewatata wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari nchini kuacha kutumia dawa za kulevya ikieleza baada ya kufanya utafiti imegundua asilimia kubwa ya wanafunzi wameathirika na matumizi ya dawa hizo hali inayowafanya kushindwa kutimiza malengo yao.
Akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa
Umma, tawi la Tanga pamoja na wadau mbalimbali, Makamu mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa, Mwanne Ismail Nchemba alisema wana
ugomvi mkubwa wa dawa za kulevya.
“Kwenye mkusanyiko wa watu hasa vyuoni na mashuleni,
watumiaji wa dawa wamo,” alisema Mwanne wakati kamati hiyo ilipofanya ziara
katika chuo hicho kilichopo Kange jijini Tanga.
Mwanne alisema malengo ya Taifa yatapotea iwapo wanafunzi
hawatakuwa na msimamo wa maisha yao wenyewe akiongeza kwamba Serikali imeweka
taratibu katika vyuo na sekondari kwa ajili ya kudhibiti dawa hizo viroba akieleza
kwamba hata wanafunzi wa shule za msingi walikuwa wanatembea na viroba mfukoni.
"Tusidanganyane kwenye mkusanyiko wa wanafunzi kuna
wanaovuta bangi na watumiaji wa dawa za kulevya. Pia suala la viroba
tumeshaanza kulishughulikia, tuko hapa kwa malengo basi iwe vizuri tukazingatia
malengo ya utumishi bora ili tuwe kioo katika jamii na serikali,” alisema Mwanne.
Kwa upande wake, mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni
mbunge wa Ukonga (Chadema) Waitara Mwita alisema taasisi nyingi za Serikali
hazitumii nafasi ya vyuo vya utumishi ikiwemo kutokufanyika kwa semina elekezi hivyo
kuna haja ya kubana matumizi kwani dunia inabadilika lazima watu waende na
wakati.
0 comments:
Post a Comment